5Wazao wa Washiloni waliorudi ni: Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.
6Kwa wana wa Zera: Yeueli. Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690.
7Kwa Benyamini walikuwa: Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
8Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya.
9Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao.