1 Wakorintho 10

Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo.

1 Corinthians 10:15 (UKJV) I speak as to wise men; judge all of you what I say.

13Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

14Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu.

15Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo.

16Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?

17Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.