1 Wakorintho 10

Wote wakabatizwa kuwa wa Mose ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari.

1 Corinthians 10:2 (UKJV) And were all baptized unto Moses in the cloud and in the sea;

1Ndugu zangu, sitaki mkose kufahamu ukweli huu kwamba baba zetu walikuwa wote chini ya wingu na kwamba wote walipita katikati ya bahari.

2Wote wakabatizwa kuwa wa Mose ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari.

3Wote walikula chakula kile kile cha roho,

4na wote wakanywa kile kile kinywaji cha roho, kwa maana walikunywa kutoka ule mwamba wa roho uliofuatana nao, nao ule mwamba ulikuwa Kristo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.