17Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu.
18Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa.
19Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu sana katika Bwana.
20Ndugu wote walioko hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
21Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe.