18Baadhi yenu mmekuwa na jeuri mkidhani kuwa sitafika kwenu.
19Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao.
20Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu.
21Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?