1 Wafalme 10

Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,

1 Kings 10:14 (UKJV) Now the weight of gold that came to Solomon in one year was six hundred threescore and six talents of gold,

12Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.)

13Mfalme Solomoni akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, kando na vile mfalme alivyokuwa amempa kwa ukarimu wake wa kifalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.

14Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,

15mbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Kiarabu na watawala wa nchi.

16Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.