11Neno la Bwana likamjia Solomoni kusema:
12“Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako.
13Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.”
14Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha.
15Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari.