1 Samweli 1

Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake.

1 Samuel 1:12 (UKJV) And it came to pass, as she continued praying before the LORD, that Eli marked her mouth.

10Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana.

11Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.”

12Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake.

13Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa

14naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.