1 Samweli 20

Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

1 Samuel 20:11 (UKJV) And Jonathan said unto David, Come, and let us go out into the field. And they went out both of them into the field.

9Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?”

10Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?”

11Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

12Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha?

13Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.