3Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.
4Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,
5tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,
6tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika.
7Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.