2 Wakorintho 3

Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.

2 Corinthians 3:14 (UKJV) But their minds were blinded: for until this day remains the same vail untaken away in the reading of the old testament; which vail is done away in Christ.

12Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana.

13Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.

14Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.

15Hata leo Sheria ya Mose inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao.

16Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana, utaji unaondolewa.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.