23Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
24Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.
25Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake.
26“Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,
27kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.