37Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.
38“Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
39Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu.
40Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
41Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu.