2 Timotheo 4

Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda.

2 Timothy 4:7 (UKJV) I have fought a good fight, I have finished my course, I have kept the faith:

5Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.

6Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia.

7Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda.

8Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.

9Jitahidi kuja kwangu upesi

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.