Matendo 13

“Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu

Acts 13:32 (UKJV) And we declare unto you glad tidings, how that the promise which was made unto the fathers,

30Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu.

31Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu.

32“Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu

33sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: “ ‘Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.’

34Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika nilizomwahidi Daudi.’

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.