Matendo 8

Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.

Acts 8:3 (UKJV) As for Saul, he made havoc of the church, entering into every house, and haling men and women committed them to prison.

1Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria.

2Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana.

3Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.

4Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda.

5Filipo akateremkia mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Kristo

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.