18Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana.
19Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.
20Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.
21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
22Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.