Kumbukumbu 1

Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema:

Deuteronomy 1:34 (UKJV) And the LORD heard the voice of your words, and was angry, and swore, saying,

32Pamoja na hili, hamkumtegemea Bwana Mungu wenu,

33ambaye aliwatangulia katika safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea.

34Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema:

35“Hakuna mtu wa kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa kuwapa baba zenu,

36isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na wazao wake nchi aliyoikanyaga kwa miguu, kwa sababu alimfuata Bwana kwa moyo wote.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.