Kumbukumbu 32

“Je, hili sikuliweka akiba na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina?

Deuteronomy 32:34 (UKJV) Is not this laid up in store with me, and sealed up among my treasures?

32Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kutoka kwenye mashamba ya Gomora. Zabibu zake zimejaa sumu, na vishada vyake vimejaa uchungu.

33Mvinyo wao ni sumu ya nyoka, sumu yenye kufisha ya swila.

34“Je, hili sikuliweka akiba na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina?

35Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza. Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza; siku yao ya maafa ni karibu, na maangamizo yao yanawajia haraka.”

36Bwana atawahukumu watu wake, na kuwahurumia watumishi wake atakapoona nguvu zao zimekwisha wala hakuna yeyote aliyebaki, mtumwa au aliye huru.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.