2“Ubatili mtupu! Ubatili mtupu!” Mhubiri anasema. “Ubatili mtupu! Kila kitu ni ubatili.”
3Mwanadamu anafaidi nini kutokana na kazi yake yote anayotaabikia chini ya jua?
4Vizazi huja na vizazi hupita, lakini dunia inadumu milele.
5Jua huchomoza na jua huzama, nalo huharakisha kurudi mawioni.
6Upepo huvuma kuelekea kusini na kugeukia kaskazini, hurudia mzunguko huo huo, daima ukirudia njia yake.