3Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.
5Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
6Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.
7Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.