11Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni.
12Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini.
13Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana,
14kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana: “Amka, wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, naye Kristo atakuangazia.”
15Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima,