15Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima,
16mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu.
17Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana.
18Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.
19Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu,