18Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.
19Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu,
20siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
21Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo.
22Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana.