6Mtu yeyote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya wale wasiomtii.
7Kwa hiyo, msishirikiane nao.
8Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru
9(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli),
10nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana.