7Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake.
8Walete wanawe na uwavike makoti,
9pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe.
10“Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake.
11Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania.