Kutoka 33

Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa.

Exodus 33:15 (UKJV) And he said unto him, If your presence go not with me, carry us not up behind.

13Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.”

14Bwana akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”

15Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa.

16Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?”

17Bwana akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.