23na kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.
24Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu
25na kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.
26Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia
27na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Bwana alivyomwagiza.