Ezekieli 16

“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta.

Ezekiel 16:9 (UKJV) Then washed I you with water; yea, I thoroughly washed away your blood from you, and I anointed you with oil.

7Nilikufanya uote kama mmea wa shambani. Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, wewe uliyekuwa uchi na bila kitu chochote.

8“ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye Agano na wewe, asema Bwana Mwenyezi, nawe ukawa wangu.

9“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta.

10Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa.

11Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako,

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.