3Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili?
4Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure!
5Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?
6Kama vile “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”
7Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Abrahamu.