14Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
15Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.
16Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka.
18Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.