1Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.
2Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
3Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.
4Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.