Mwanzo 28

tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu.

Genesis 28:7 (UKJV) And that Jacob obeyed his father and his mother, and was gone to Padanaram;

5Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau.

6Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,”

7tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu.

8Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani.

9Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.