Mwanzo 39

Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani.

Genesis 39:16 (UKJV) And she laid up his garment by her, until his lord came home.

14akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele.

15Aliposikia kelele za kuomba msaada, akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia nje.”

16Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani.

17Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki.

18Lakini mara nilipopiga kelele kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu akakimbia nje ya nyumba.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.