1Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi.
2Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.”
3Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’
4Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula.