6Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
8Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
9Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.