Yeremia 29

Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Jeremiah 29:13 (UKJV) And all of you shall seek me, and find me, when all of you shall search for me with all your heart.

11Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Bwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

12Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza.

13Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

14Nitaonekana kwenu,” asema Bwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema Bwana.

15Mnaweza mkasema, “Bwana ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.