17Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.
18Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.
19Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.
20Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.
21Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu.