21Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
22Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu.
23Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
24Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
25Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?