25Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu?
26Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
27Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
28“Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo.