11Je, faraja za Mungu hazikutoshi, au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?
12Kwa nini moyo wako unakudanganya, na kwa nini macho yako yanangʼaa,
13ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?
14“Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu?
15Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake,