11Huwatoa watoto wao nje kama kundi; wadogo wao huchezacheza.
12Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi.
13Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani.
14Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
15Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?