2Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia?
3Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa.
4Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio.
5Walifukuzwa mbali na watu wao, wakipigiwa kelele kama wevi.
6Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, kwenye majabali na mahandaki.