17Mimi nami nitakuwa na la kusema; mimi nami nitasema lile nilijualo.
18Kwa kuwa nimejawa na maneno, nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma;
19ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka.
20Ni lazima niseme ili niweze kutulia; ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu.
21Sitampendelea mtu yeyote, wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote;