6Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua.
7Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’
8Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu.
9Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.
10“Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi; mimi nami nitawaambia lile ninalojua.