26Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu.
27Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata,
28nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.
29Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake.
30Mimi na Baba yangu tu umoja.”