8Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9“Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu.
10Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
11Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili.
12Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi.