6Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho.
7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’
8Upepo huvuma popote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.”
9Nikodemo akamuuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
10Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya?