8Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.”
9Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
10Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.”
11Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ”
12Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”