55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.
58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.”
59Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.